June 29, 2018


Uongozi wa klabu ya Simba umetoa tamko kuhusiana na kiungo wa Mtibwa Sugar, Hassan Dilunga aliyehusishwa kujiunga na timu hiyo ambayo ni bingwa wa Ligi Kuu msimu wa 2017/18.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa klabu, Haji Manara, amesema tetesi zilizoelezwa hawezi kuzizungumzia huku akisema kama wakiwa kwenye mipango naye watamtangaza.

Manara ameeleza kuwa Simba haifanyi usajili wa kimyakimya na badala yake inatangaza moja kwa moja na si kama ambavyo watani zao wa jadi Yanga.

Ofisa huyo amefunguka na kusema anashangaa timu inayosema kuwa wanasajili kimyakimya (akimaanisha Yanga) lakini pia akieleza wao kama Simba hawana muda wa kuficha jambo lolote lile.

Mapema jana taarifa zilizuka kuwa mabosi wa Simba tayari wameshaanza mazungumzo na Dilunga ambaye pia inaelezwa kuwa Yanga wanahitaji huduma yake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic