June 29, 2018



Katibu Mkuu wa CECAFA. Nicholas Musonye ameibuka na kutoa kauli tata juu ya Yanga kuhusiana na kujiondoa kwenye mashindano ya KAGAME.

Musonye amewatupia lawama kimafumbo Yanga akiisema imeamua kujitoa kwenye mashindano ya KAGAME lakini ilienda kushiriki michuano ya Karata nchini Kenya akimaanisha SportPesa Super CUP.

Kauli hiyo imekuja kufuatia hivi karibuni uongozi wa Yanga ulituma maombi kwenda TFF ukiomba kujiondoa kushiriki mashindano hayo ili kuwapa nafasi wachezaji wake kwa ajili ya kupumzika.

Michuano hiyo inaanza rasmi leo kwa mechi tatu kupigwa ambapo saa 8 mchana JKU ya Zanzibari itaanza kibarua chake dhidi ya Vipers SC kutoka Uganda.

Baadaye saa 10 mechi ya rasmi ya ufunguzi itakuwa baina ya mabingwa watetezi, Azam FC dhidi ya Kator FC kutoka Sudan Kusini. Baada ya mechi hiyo majira ya saa 1 jioni, Singida United itacheza na APR ya Rwanda.

5 COMMENTS:

  1. Sportspesa inajulikana ipo Kagame inakurupuka .Musonye atangaze mwakani Kagame Cup inachezwa wapi Kama anajua anachofanya

    ReplyDelete
  2. Huyu Jaluo uwezo wake wa kufikiri ni mdogo,SportPesa wana maslahi na Yanga kutokana na udhamini wao kwa hiyo walikuwa hawana jinsi bali kushiriki hata kama ni kwa shingo upande sio CECAFA ambao wanazifanya timu kama mashine zao za kuingiza kipato tena hasa timu za Tanzania na ndio maana wakawapanga Yanga na Simba kundi moja ili watengeneze hela haraka haraka waweze kujilipa posho na kugharamia baadhi ya mahitaji wakihofia kama wangepangwa makundi tofauti basi huenda wasingekutana na matokeo yake mipango yao isingetimia.
    Mwaka huu Musonye amechambia jani la mgomba

    ReplyDelete
    Replies
    1. Point of correction.... Si kila mkenya ni Jaluo.. Rekebisha hilo la sivyo yote utakayoongea yataonekana pumba!

      Delete
    2. Uko sahihi.watafute vyanzo vingine vya mapato

      Delete
  3. Hata cecafa ni michuano ya hasara kabisa na haina tofauti na kombe la kuku

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic