Muonekano wa Uwanja wa Simba huko Bunju baada ya hatua ya uwekwaji kifusi kukamilika kabla ya kipindi cha masika kuanza. |
Uwanja wa Simba uliokuwa umeanza kujengwa maeneo ya Bunju jijini Dar es Salaam umevamiwa na wananchi kwa kuanza kutumika kama sehemu ya malisho ya mifugo kutokana na nyasi nyingi kuota.
Kwa mujibu wa Radio One, mmoja wa raia aliyepo maeneo hayo amesema mpaka sasa hakuna chochote kinachoendelea na badala yake wananchi wa maeneo hayo wamekuwa wakitumia eneo hilo kuchungia mbuzi.
Hivi karibuni, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara, alisema ujenzi huo unaendelea kama kawaida na akisema kuwa kuelekea msimu ujao mambo yanaweza yakawa shwari kwa kiwanja hicho kutumika kwa ajili ya mazoezi.
Mlinzi aliyekabidhiwa kulinda eneo hilo amesema viongozi wa Simba wamekuwa watata kwani tangu akabidhiwe kulinda eneo hilo amesema mabosi wake hawajawahi kwenda kufuatilia chochote.
Mlinzi huyo amefunguka na kusema mara ya mwisho alipokea simu ya Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ikieleza kuwa atakuja mtaalamu wa ujenzi lakini alionekana kwa siku moja pekee na hakuweza kuonekana tena baadaye.
Naomba waandishi muandike sana kuhusu uwanja labda viongozi wataukumbuka! Yaani shule za msingi tu zina viwanja Simba tunashindwaje!!
ReplyDeleteHII NI AIBU VIONGOZI WETU SIMBA KWANINI MNAJISAHAU ? WHY? HAMNA UCHUNGU?
ReplyDelete