WACHEZAJI 14 YANGA WAANZA MAJARIBIO WAKATI KIKOSI KIKIJIANDAA KUKIPIGA NA GOR MAHIA
Kikosi cha Yanga kimeanza rasmi mazoezi jana katika Uwanja wa Polisi, Kurasini jijini Dar es Salaam baada ya kambi waliyokuwa wamepewa wachezaji kumalizika.
Ofisa Habari wa klabu hiyo, Dismas Ten, amesema kuwa jumla ya wachezaji 14 waliokuja kufanya majaribio na Yanga wameanza wakiwa chini ya Kocha Mkuu, Mkongomani, Mwinyi Zahera.
Ten ameeleza wachezaji hao ndiyo kwanza wameanza kujinoa na akisema kama benchi la ufundi litaridhishwa nao wataweza kusajiliwa.
Kikosi hicho kimeanza kujifua kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya Kombe la Shirikisho ambapo itakuwa ina kibarua dhidi ya Gor Mahia FC, Julai 18 2018 nchini Kenya.
Tayari wachezaji wengi wamewasili huku baadhi wakiwa hawajafika na bila shaka kuanzia kesho na kuendelea wote watakuwa wamewasili.
0 COMMENTS:
Post a Comment