June 27, 2018


Croatia na Argentina zimefuzu kucheza hatua ya mtoano katika 16 za michuano ya Kombe la Dunia huko Urusi.

Argentina wamemaliza michezo yao kwenye kundi D wakiwa na alama 4 katika nafasi ya pili kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Nigeria.

Mabao ya Argentina yamewekwa kimiani na Lionel Messi mapema katika dakika ya 14 huku la pili likifungwa na Marcos Rojo mnamo dakika ya 86 ya kipindi cha pili. 

Bao pekee la Nigeria liliwekwa kimiani kwa mkwaju wa penati kupitia kwa Victor Moses katika dakika ya 51 ya kipindi cha pili.

Wakati huo Ufaransa pamoja na Denmark zimefuzu kuingia mtoano baada ya sare ya kutofungana leo mchana katika mchezo wa kundi C.

Kutokana na matokeo hayo, Ufaransa sasa itakipiga dhidi ya Argentina katika hatua ya mtoano huku Denmark ikicheza dhidi ya Croatia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic