Na George Mganga
Wakati michuano ya kombe la KAGAME ikianza leo jijini la Dar es Salaam, uongozi wa Simba umetangaza kuwa utawakosa baadhi ya wachezaji wake muhimu.
Kwa mujibu wa Daktari wa timu hiyo, Yassin Gembe, amesema kuwa wachezaji Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, John Bocco, Salim Mbonde na Aishi Manula watakosekana kutokana na kusumbuliwa na majeraha.
Gembe amesema hali za wachezaji hao kiafya si nzuri hivyo watapasw kupumzika ili kujiandaa na mashindano ya ligi kwa msimu ujao hivyo hawatoweza kushiriki KAGAME.
Mbali na majeruhi hao, wachezaji wengine ambao ni Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Haruna Niyonzima na Emmanuel Okwi wao wapo likizo makwao hivyo uwezekano wa kushiriki KAGAME hautokuwepo.
Uongozi umesema kuelekea msimu ujao wa ligi wachezaji wote waliopo likizo watakuwa wamerejea kikosini huku ambao ni majeruhi hali zao zikitarajiwa kurejea vema kutokana na matibabu wanayopatiwa.
Mipango safi kabisa . Wengine wanacheza KAGAME na wengine wanapewa nafasi ya kupimzika. Hongereni Viongozi wa Simba
ReplyDelete