June 3, 2018


Wakati michuano ya SportPesa Super Cup ikianza kurindima leo Kenya, uongozi wa Simba kupitia Kaimu Rais wake, Salim Abdallah 'Try Again' umesema kuwa wachezaji watatu wataondoka leo nchini humo.

Tyr Again ameeleza kuwa wachezaji hao watatu ambapo wawili ameficha majina yao, wataondoka kwenda kukipa nguvu kikosi hicho huku mmoja wao akiwa ni Shiza Kichuya.

Simba itaanza kutupa karata yake ya kwanza siku ya Jumatatu dhidi ya Kariobang Sharks kuanzia mida ya saa 9 mchana.

Wakati huyo Yanga inaanza kibarua chake leo kwa kukipiga na Kakamega ikifungua rasmi pazia la michuano hiyo kuanzia saa 7 kamili za mchana.

Mshindi wa kombe hilo ataenda England kukipiga na Everton katika Dimba la Goodson Park.





2 COMMENTS:

  1. LETENI TAARIFA MPYA HIZI MBONA NI ZA ZAMANI NANI ASIYEJUA YANGA WANACHEZA LEO

    ReplyDelete
  2. Pia watueleze liliwazuia Bocco, Okwi na na Asante kwasi kujiunga ambao ni uti wa mgongo wa mafanikio

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic