June 27, 2018


Brazil wazee wa samba wanaingia kibaruani tena leo katika mchezo wa Kundi E dhidi ya Serbia kuanzia saa 3 kamili usiku kuelekea hatua ya kufuzu kuingia 16 bora.

Brazil wanaingia kibaruani wakiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Costa Rica katika dakika za mwisho katika mchezo uliopita.

Mbali na Brazil, Switzerland nao watakuwa wana kibarua dhidi ya Costa Rica katika mchezo huo wa kundi E. 

Katika kundi hilo Brazil na Uswiz ndizo zenye nafasi kubwa ya kusonga mbele kutokana na msimamo ulivyo kwenye kundi ambapo Brazil wana alama 4 na Uswizi wana 4 pia.

Mechi zingine zitakazopigwa mapema saa 11 jioni kutoka kundi F ni Mexico watakuwa wanakipiga dhidi ya Sweden wakati pia Korea Kusini wakicheza dhidi ya Ujerumani,

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic