June 27, 2018


Wakati aliyekuwa mshambuliaji hatari wa Gor Mahia FC, Meddie Kagere kufanikiwa kujiunga na Simba kwa kusaini mkataba wa miaka miwili, uongozi wa Yanga nao umetoa tamko lake kuhusiana na mchezaji huyo.

Hivi karibuni kabla ya Kagere kuelekea Simba, Yanga walikuwa wa kwanza kuanza kuhusishwa kumnyatia mchezaji huyo kutokana na kiwango kikubwa alichokionesha kwenye mashindano ya SportPesa Suoer CUP.

Kupitia Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, amesema kuwa Yanga haikuwa na mazungumzo yoyote juu ya kumsajili mchezaji huyo kwani mipango yao inaenda kimyakimya.

Ten ameeleza kuwa wanachama na wapenzi wa Yanga wawe na subira kwani mpaka sasa hawajataja nani na nani wamemsajili hivyo wakati ukifika kila kitu kinawekwa hadharani.

Kikosi hicho jana kimeanza rasmi mazoezi katika Uwanja wa Polisi Kurasini, Dar es Salaam kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya KAGAME yanayotarajiwa kuanza Juni 29 wiki hii.

6 COMMENTS:

  1. Kimya kimya Fc mnajaribu kuzuia mafuliko kwa viganja vya mikono,yajayo yatawasononesha zaidi.Mwaka huu mtapata taabu sana.

    ReplyDelete
  2. Tarimba analaumu Simba imewachukua wachezaji "wao" na Dismas msemaji wa Yanga anadai hawakuwa na habari nao. Nani anasema ukweli.

    ReplyDelete
  3. Haya TEN anatema hawakuwa na mazungumzo na Kagere, huku Tarimba analaumu Simba kunyanganya mchezaji waliomtaka kumsajili. Tarimba hasemi ukweli. Ten amesema ukweli. Lakini pia suala hapa ni pesa. Toa pesa ya kutosha mchezaji atasaini sio kupiga porojo gazetini.

    ReplyDelete
  4. Uongozi Tarimba unakushinda sasa na ulikushinda miaka ya nyuma bakia njia kuu Sportipesa. Utaharibu kibarua chako Halima

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic