YANGA WATOA KAULI HII KWA WACHEZAJI WATAKAOPATA OFA YA KUKIPIGA NJE YA TANZANIA
Na George Mganga
Mkuu wa Kamati ya Usajili wa klabu ya Yanga, Hussin Nyika, amesema kamwe hawatoweza kuwabania wachezaji wao watakaopata ofa za kucheza nje ya Tanzania.
Nyika amefunguka na kueleza hayo mara baada ya tetezi kueleza kuwa Mshambuliaji wao, Emmanuel Martin anawindwa na Waasland Beveren inayoshiriki Ligi Kuu Ubelgiji.
Nyika amesema haitawakataza wachezaji kwenda kukipiga kimataifa kwani watakuwa wanalinufaisha taifa na ni haki yao kutafuta riziki.
Kiongozi huyo ameweka wazi kuhusiana na taarifa zilizoelezwa kuhusiana na Martin kuhitajia Ubelgiji akisema watalieleza zaidi wakati ukifika huku akisema kuna wachezaji wengine wanaowinda na timu za nje ya Tanzania.
0 COMMENTS:
Post a Comment