June 27, 2018


Na George Mganga

Baada ya Simba kufanikiwa kupata saini ya mchezaji hatari aliyekuwa Gor Mahia FC, Meddie Kagere kwa kumsainisha miaka miwili, uongozi wa Yanga umetaja sababu za kuhindwa kumalizana naye.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Yanga, Hussein Nyika, amefunguka na kueleza kuwa timu yao huwa haisajili wachezaji ambao hawawezi kudumisha viwango vyao kwa muda mrefu.

Nyika amesema Yanga inapendelea zaidi kusajili wachezaji ambao wanaweza wakakaa kwa takribani miaka mitatu mpaka minne huku viwango vyao vikiwa katika hali ileile.

Kwa mujibu wa Radio One, Nyika amefunguka hayo kutokana na mipango ya awali iliyoelezwa kuwa Yanga ilikuwa kwenye harakati za kutaka kumsajili mchezaji huyo lakini Simba ikawazidi kete kwa kuweza kumuwahi.

Mwenyekiti huyo wa usajili ameeleza umri wa Kagere ni mkubwa hivyo mipango ya kumalizana naye haikuwezekana sababu asingeweza kudumu zaidi.

Aidha jana Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, alikanusha uwepo wa tetesi zilizoeleza kuwa klabu ilikuwa inahitaji kumsajili Mshambuliaji huyo hatari aliyekuwa Gor Mahia.

11 COMMENTS:

  1. Hahahahahahaahaaaaah.. kwel mnapata shida sana mwaka huu..

    ReplyDelete
  2. Kutokana na matamko hayo yasiyokuwa mantiki ambayo sikweli hata kidogo, yanga inazidi kujiaibisha. Kwanini hawasemi keeli kuwa wameshindwa alichokitaka Ksgere? Sungura alipozikosa zabibu alisemaaje? Yanga mwaka huu mmekalia kuti kavu na huku ligi ikikaribia hamjui la kufanya. Mmebakia kuwaandama kila waliokukataeni. Fanyeni haraka kabla halijafungwa dirisha

    ReplyDelete
  3. Kevin Yondani hana mkataba. Kama Nyika anasema kweli wasimpe mkataba kwa sababu kiumri amemzidi Kagere miaka miwili. Hivi Ronaldo akija Yanga mtamkataa kwa sababu ana miaka 33?
    Nyika alimsajili Ngoma akiwa majeruhi leo anadai Kagere ana umri mkubwa.Kwani wamejua umri wake leo. Gor Mahia wanalia kwa kushindwa kumbakisha .

    ReplyDelete
  4. Salamba pia walishindwa kumsajili kwa sababu ana umri mkubwa. Ukweli siku zote humuacha mtu huru. Nyika akiri tu kwamba yake fupi.

    ReplyDelete
  5. Salamba pia walishindwa kumsajili kwa sababu ana umri mkubwa. Ukweli siku zote humuacha mtu huru. Nyika akiri tu kwamba kamba yake fupi.

    ReplyDelete
  6. Viongozi wetu Yanga majibu gani mnayotoa ya kitoto? Nyika anaeleza vyake, Ten anasema hawajawahi kumuhitaji Kagere, na Tarimba anasema wamemuhitaji yupo kwenye mipango ya kusajiliwa Yanga ila Simba wametutibulia dili na kulaumu Simba hawana uwezo wa kuscout wachezaji. Jamani majibu ya ovyo kabisa. Kwanini mnaiaibisha Yanga mmelazimishwa kusema si mkae kimya tuu

    ReplyDelete
  7. Nakubaliana na hoja ya kuwana kukosi kitakachokaa pamoja kwa muda mrefu kwa maana nyingine kuwa na strategic team badala ya timu ya pro active team laini kuna mahai kiongozi umejichanganya kdg nanukuu 'Mwenyekiti huyo wa usajili ameeleza umri wa Kagere ni mkubwa hivyo mipango ya kumalizana naye haikuwezekana sababu asingeweza kudumu zaidi' yumkini moja ya maswali ya usajili ni UMRI WAKO? kifupi sio suala la umri maana msingeanza mipango ya KUMALIZANA NAYE, mngemalizana naye hili la umri lisingekuwepo

    ReplyDelete
  8. kauli za kushindwa hizo mbona Kelvin yondan ana umri mkubwa bado wanamtaka # watapata tabu xana

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kelvin Yondani alisajiliwa Yanga takriban miaka saba iliyopita akiwa bado ana umri mdogo huwezi toa Kigezo cha umri wa Yondani kwa sasa kumlinganisha na Kagere wakati amedumu na timu muda mrefu ilhali huyu anakuja kuziba nafasi za vijana ambao wangedumu na timu muda mrefu

      Delete
  9. kauli za kushindwa hizo mbona Kelvin yondan ana umri mkubwa bado wanamtaka # watapata tabu xana

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic