June 27, 2018


Fedha za Mo sasa ni kufuru Simba. Mambo sasa ni safi kwa aliyewahi kuwa kipa wa Yanga, Diego Munish ameweza kumalizana na mabingwa wapya wa klabu hiyo ikielezwa amesaini mkataba wa miaka miwili.

Dida ameungana na Haruna Niyonzima ambaye aliwahi kucheza naye miaka kadhaa iliyopita wakati akiwa klabu ya Yanga.

Ujio wa Dida katika kikosi cha Simba ni mahususi kuja kumpiga tafu Aishi Manula kuanzia kwenye michuano ya KAGAME inayoanza Juni 29 2018 wiki hii.

Kipa huyo imeelezwa atakuwa mdabala wa Manula katika mashindano hayo baada ya kupewa mapumziko kujiandaa na mashindano ya Ligi Kuu Bara msimu ujao.

Usajili wa Dida kujiunga Simba umekuja mara baada ya mshambuliaji hatari Meddie Kagere kutoka Gor Mahia kusainishwa pia miaka miwili jana.

3 COMMENTS:

  1. Duuuh kweli Simba kapania

    ReplyDelete
  2. Hahahaha that's good Simba oyeeeee

    ReplyDelete
  3. Wow simba looks like next season is going to do something good, than what it done last season

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic