July 5, 2018








Kampuni ya mawasiliano ya imezindua huduma mpya kwa wateja wake wanatuma na kupokea pesa kupitia Airtel Money.

 Wateja wa Airtel wanaotumia huduma hiyo kwa sasa wataweza kutuma na kupokea pesa bure kabisa bila makato yoyote.

 Akizungumza  katika uzinduzi huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo nchini, Mkurugenzi wa masoko, Isack Nchunda alisema: “Tuna furaha kubwa kuona ongezeko la watumiaji  wa Airtel  Money  wanaongezeka kila siku, tunaamini kuwa malengo  serikali kuhakikisha  inafanikisha  upatikanaji wa huduma ya kifedha  kwa kila mwananchi inalekea kupata mafanikio makubwa.

 “Leo Airtel tunazindua huduma hii inayojulikana kama Hakatwi mtu hapa, tuma pesa bure ili kuendelea kuunga mkono juu za serikali  na kuwawezesha wateja wetu zaidi ya milioni kumi nchini kuweza kutuma na kupokea pesa bure,” alisema Nchunda.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic