July 5, 2018


Na George Mganga

Kocha Mkuu wa Gor Mahia FC, Dylan Kerr, amefunguka kuhusiana na kiungo wa timu yake, Francis Kahata, kuhusishwa kutimkia katika klabu yake ya zamani ya Simba.

Kerr ameeleza kuwa hana tatizo na mabosi wa Simba kumsajili mchezaji ikiwa ni takribani wiki moja na siku kadhaa zimepita tangu wamalizane na aliyekuwa straika wa kikosi cha Gor Mahia, Meddie Kagere.

Kiungo wa Gor Mahia FC, Francis Kahata

Kerr ameeleza kama Simba wanahitaji kumsajili Kahata hawapaswi kutumia njia za kinyemela na badala yake wanapaswa kufuata taratibu rasmi kwa kufanya mawasiliano na uongozi wa klabu waweze kufika nao mwafaka.

Kocha huyo aliyewahi kusakata kambumbu na klabu za Leeds United, Reading na zinginezo huko England amewataka Simba kufanya hivyo ili kuonesha ueledi kutokana na taratibu za usajili zinavyotaka.

"Kama Simba wanamtaka Kahata wanapaswa kuzungumza na mabosi wangu, si kumnyemelea kwasababu haileti maana nzuri, ni kiungo mzuri katika kikosi chetu na bado ana mkataba na klabu, kama wamefurahishwa naye, vema wakafanya mazungumzo na viongozi ili waweze kumalizana" amesema Kerr.

Kocha Kerr yupo hapa nchini jijini Dar es Salaam na timu ya Gor Mahia kwa ajili ya mashindano ya CECAFA KAGAME CUP yanayoendelea hivi sasa ambapo leo majira ya saa 12 jioni, watakuwa wanashuka dimbani kucheza dhidi ya AS Ports ya Djibout.






4 COMMENTS:

  1. Kocha huyu anaongea sana kuhusu Simba kuliko timu yake ambaye inakabiliwa na mgogoro mkubwa kwa wachezaji kutolipwa haki zao kama allowances mishahara na pesa za Sports pesa Cup. Yupo obsessed nä Simba.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kocha Kerr anaonekana ana kitu fulani kinamtatiza anapoifikiria Simba. Hili la mchezaji kutakiwa na Simba yeye wala lisingemuhusu. Muda ukifika kwavyovyote Simba itakamilisha mipango hiyo kwa kufuata taratibu zote , hivi Leseni ya kucheza wataipataje pasipo kupitia viongozi wa soka wa Kenya? Kerr atulie tu.

      Delete
    2. Kerr kajibu kama alivyoulizwa na mwandishi..sidhani kama Kerr alimfuata mwandishi bali mwandishi amemfuata Kerr na kutoa maoni yake..sioni tatizo la Kerr

      Delete
  2. Tatizo ni kocha anapo comment uvumi .Mpaka sasa hakuna uhakika wa habari yenyewe. Simba kama wanamhitaji Kahata na ana mkataba watawasiliana na Gor Mahia.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic