Kampuni Star Times imeingia mkataba wa wa kimaudhi na kampuni ya Trend Solar inayojihusisha na uzalishaji wa Umeme wa Jua kwa kuonyesha matangazo yake kupitia luninga ya kampuni hiyo.
Star Times ambao kwa sasa wanaonyesha michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini Urusi imepewa jukumu hilo la kutoa huduma ya matangazo kwa njia ya kidigitali kutokana na na kuwa na watumiaji wengi barani Afrika ikiwa ni zaidi ya milioni kumi.
Akizungumza na katika uzinduzi huo uliofanyika jana jijini Dar na kuhudhuriwa na Balozi wa Uingereza nchi, Saraha Crooke, Mtendaji Mkuu wa Star Times, Walker Wang alisema kuwa kushirikiana na Trend Solar ni hatua ya msingi kwa kuwa kampuni yake inawafikia watu wengi walioko vijijini hasa wale ambao wamekuwa hawapati umeme.
Kushirikiana na Trend Solar ni hatua ya msingi kwani Star Times tutawafikia watu wengi walioko vijijini hasa wale ambao hawapato umeme wa gridi, tunayo furaha kubwa kushirikiana na timu hii katika mradi huu mkubwa wa luninga za kidigitali ili kuwapatia fursa Watanzania wengi zaidi kufurahia maudhui na vipindi vyetu wakiwa na familia zao,” alisema Wang.
Kwa upande wa Mtendaji mkuu wa Trend Solar, Irfan Mirza ambaye ndiyo mwanzilishi alisema kuwa: “Kupitia Trend Solar tunawaondolea watu wetu tatizo la kusahaulika kwenye maendeleo ya kidigitali kwa kuwapatia Simu ya gharama nafuu.
"Intaneti ya bure na vifaa vya kuchajia nyumbani kutokana na umeme huu ambao hautumi gridi za taifa kwa kupitia mpango huu wa kisasa wa umeme ambao utasaidia jamii kubwa ya Afrika.”
MAMBO NI MOTOO...
ReplyDelete