AKIWA BADO YUPO KWAO RWANDA, NIYONZIMA AIBUA HASIRA ZA WANASIMBA
Baadhi ya mashabiki wa klabu ya Simba wameshangazwa na kiungo Mrwanda, Haruna Niyonzima kutokana na kitendo chake cha kuchelewa kuripoti nchini.
Niyonzima alipewa likizo ya kurejea kwao Rwanda kutokana na matatizo ya kifamilia ambayo ilimalizika Julai 20 lakini mpaka sasa hajarejea Tanzania.
Kutokana na maamuzi ya mchezaji huyo kuendelea kusalia kwao Kigali, Rwanda, mashabiki hao wameshangazwa na mchezaji huyo wakihoji kwanini afanye hivyo ilihali stahiki zote anapata.
Shabiki mmoja ambaye jina lake hakutaka litajwe, amesema Niyonzima amefanya maamuzi ambayo si mazuri na kueleza kuwa anaiangusha klabu na wanasimba wote waliomwamini wakati anasajiliwa.
"Kusema ukweli Niyonzima anafanya kitu ambacho si kizuri ukizingatia hata uongozi hauelewi kipi kimempata huko, ni vema akaeleza shida ni nini ikiwezekana aweze kusaidiwa" alisema shabiki huyo.
Wakati Niyonzima akiwa kwao Rwanda, kikosi cha Simba kipo nchini Uturuki ambako kimeweka kambi ya wiki mbili kwa ajili ya maandalizi ya tamasha la Simba Day na Ligi Kuu Bara msimu ujao.
Nioziama pengine uoga ndio unaomsumbua. Inawezekana kachungulia pale Simba na viungo walivyojazana panakatisha tamaa.kuanzia muzamir,Dilunga,Mkude,
ReplyDeleteNdemla,ingizo jipya la mzambia,kaheza,kapombe,yaani pale Simba nafasi za wachezaji wa kiungo ni balaa ni vita ila miaka yote kwa wenye kuijua Simba ni kwamba SIMBA ni kiungo na kiungo ndio timu ya Simba sishangai kuona wanasimba wakimlilia Niozima, Simba kwa kawaida wana mahaba na wachezaji wa kiungo.
Mchezaji anapaswa kujitambua. Niyonzima anaikosea Simba. Niyonzima ameumia hakuweza kuitumikia Simba ipasavyo. Ni Simba iliyomgharamia matibabu yake hadi kumpeleka India kwa matibabu zaidi. Hilo tupu ni jambo kubwa la kuishukuru Klabu. Badala yake ni kufanya mambo ya kihuni kwa Klabu? Haipendezi hata kidogo. Mchezaji kama huyu ni kumfungulia milango aondoke. Ni bad influence. Unadhani ana mapenzi kweli na Simba?
ReplyDeleteTuwarudishie Niyonzima waturudishie Ajib. Wote hawana mapenzi na timu zao mpya. Ila huyu
Delete