LEBREON JAMES AMCHANA RAIS TRUMP KUHUSIANA NA KUIGAWA MAREKANI
Mchezaji wa mpira wa kikapu wa timu ya Los Angeles Lakers, James LeBron, amesema Rais wa Marekani, Donald Trump, anaitumia michezo kuwagawa Wamarekani.
Ameyasema hayo wakati akifungua shule yake aliyoifungua kwa fedha yake iitwayo ‘I Promise’ huko Akron, Ohio, akinukuu kauli ya Trump kwamba mchezaji yeyote wa soka la National Football League anayepiga goti wakati wimbo wa taifa ukipigwa, afukuzwe.
James alisema michezo isitumike kuwagawa watu, bali iwaunganishe, kwani ni katika michezo ndimo amewahi kukutana na watu wengi weupe, wakaanza kuwasiliana na kuelewana.
0 COMMENTS:
Post a Comment