July 5, 2018


Uongozi wa klabu ya Mtibwa Sugar umesema utakaa faradha na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ili kuona namna gani wanaweza wakapata nafasi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Kwa mujibu wa taarifa zilizokuja kutoka CAF, zimeeleza kuwa Mtibwa wanapaswa kulipa faini ya dola za kimarekani 1500 ili wapate nafasi hiyo, sambamba na gharama za fidia kwa klabu ya Santos inayoshiriki Ligi Kuu Afrika Kusini.

Kwa mujibu wa Msemaji wa klabu hiyo, Thobias Kifaru, amefunguka na kusema watafanya mazungumzo na TFF ili kuweza kumaliza tatizo kwa namna yoyote ile ili waweze kupata nafasi hiyo ya ushiriki.

Kifaru ameeleza kuwa kinachotakiwa hivi sasa ni kuzungumza na TFF ili kuweza kufikia mwafaka akiamini atapata msaada kinagaubaga ili wapate fursa hiyo adhimu ya kuweza kushiriki mashindano hayo makubwa.

Ikumbukwe Mtibwa ilipewa adhabu ya kutoshiriki michuano ya CAF kwa miaka mitatu katika ngazi ya klabu baada ya kushindwa kusafirisha timu kucheza mchezo wa marudiano dhidi ya Santos.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic