July 5, 2018


Na George Mganga

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema kuwa litaanza kulipa taratibu deni la takribani zaidi ya shilingi za Kitanzania, milioni 50 ambalo wanadaiwa na Kampuni ya Ulinzi (Kiwango Security).

Hatua hiyo imekuja kufuatia kampuni kuondoa walinzi wake wote kwenye ofisi hizo zilizopo mitaa ya Karume, Ilala, Dar es Salaam pamoja na kwenye makazi ya Rais wake, Wallace Karia.

Kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao, amesema watajitahidi kulipa deni la kampuni hiyo kwa taratibu za kiofisi ili walinzi hao waweze kurejea tena kuendelea na kazi kama mwanzo.

Kidao amekiri kweli wanadaiwa na hivyo itawapasa waanze kulilipa deni hilo taratibu mpaka watakapolikamilisha ili huduma iendelee.

Ikumbukwe siku kadhaa zilizopita, Mwenyekiti wa Uendeshaji katika kampuni hiyo, Sunday Marwa, alisema wameondoa wafanyakazi wao na hawatoweza kuwarudisha mpaka pale watakapolipwa fedha zao.

Chanzo: Radio One

1 COMMENTS:

  1. Kwa nini rais wa TFF alipiwe ulinzi na TFF?haya ni matumizi mabaya ya fedha za shirikisho.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic