BAADA YA KUWAONGEZEA MIKATABA WAWILI KWA MPIGO, MTIBWA YATOA KUHUSIANA NA USAJILI WA NJE
Baada ya kuwaongezea mikataba ya miaka miwili wachezaji Dickson Job na Kibwana Shomari, uongozi wa Mtibwa umesema hautasajili wachezaji wa nje ya Tanzania.
Kupitia Msemaji wa klabu hiyo Thobias Kifaru, amefunguka na kusema wao sera ya kukuza vijana na ndiyo wameingia mkataba mwingine na wachezaji hao kuendelea kuichezea Mtibwa.
Kifaru ameeleza kuwa wao wamekuwa na utamaduni wa kutengeneza vijana mpaka wanakuwa na soko la kuweza kuwauza baadaye, wataendelea kuwatumia na hata katika mashindano ya kimataifa watacheza wenyewe.
Leo mapema Mtibwa imewasainisha Shomari na Job ambao wanaichezea timu ya taifa ya vijana ya Serengeti Boys kuendelea kusakata kabumbu katika klabu hiyo iliyopo Manungu.
Nimeupenda Utaratibu Wenu, Mmeona Mbali Cos Hatuwez Kupata Tim Ya Taifa Iliyo Bora Kama Hatuwajali Wazawa, Shikamoni Mtibwa Sugar Kwa Kua Wazarendo!
ReplyDeleteHongera Mtibwa Sugar kwa Ujasiri huu wa kuwathamini wazawa....kwamba timu itaundwa na wazawa pekee kwa mashindano ya ndani na ya kimataifa mmethubutu!
ReplyDelete