GOR MAHIA BILA KAGERE YAENDA SARE TENA MICHUANO YA KAGAME
Kikosi cha Gor Mahia kimeenda sare ya 2-2 kwa mara ya pili katika mchezo wa michuano ya KAGAME dhidi ya Lydia Ludic ya Burundi.
Sare hiyo kwa Gor Mahia imekuwa ya pili mara baada ya mchezo wa kwanza dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda kwenda kwa matokeo kama ya leo ya 2-2.
Ukaichana na mechi hiyo, AS Ports ya Djibout nayo imeenda sare ya bao 1-1 na Rayon Sports kutoka Rwanda.
Baada ya mechi hizo za hatua ya makundi kukamilika, AS Ports ya Djbout ipo kileleni ikiwa na alama 4 huku Gor Mahia ikifuatia nafasi ya pili ikiwa na alama mbili, vilevile Rayon ikiwa imejikusanyia alama mbili kwenye nafasi ya tatu.
Lydia Ludic kutoka Burundi imeshika mkia ikiwa na alama moja pekee kwenye msimamo huo wa kundi B.
Hiyo Laana Ya Kuifunga Simba Sc Ina Watesa, Na Tuna Mtaka Tena Jack Twisenge!
ReplyDelete