July 6, 2018



Kikosi cha timu ya taifa ya Brazil kimeyaaga mashindano ya Kombe la Dunia kwa kukubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Ubelgiji.

Walikuwa ni Ubelgiji walioanza kutikisa nyavu za Brazil mnamo dakika ya 13 tu ya mchezo kupitia kwa Fernadinho ambaye alijifunga kwa mpira wa kichwa.

Ubelgiji walikuja tena kambani na kuweka bao la pili kwa mkwaju mkali ulioenda moja kwa moja nyavuni kupitia kwa Kevn De Bruyne kwenye dakika ya 31 kipindi cha kwanza.

Licha ya kuamka kwa kasi kipindi cha pili huku wakiutawala mchezo kuliko Ubegiji, Brazil walikosa nafasi nyingi ambazo kama wangezitumia vema wangeweza kupindua matokeo.

Mnamo dakika ya 76, Renato Agusto aliweza kuipatia Brazil bao la kufutia machozi na kuufanya ubao wa matokeo kuwa 2-1.

Baada ya kufunga bao hilo Brazil walionekana kupigana kufa na kupona ili kusawazisha lakini mpaka dakika 90 zinaisha walikuwa nyuma kwa mabao hayo mawili kwa moja.




















0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic