July 1, 2018


Imeripotiwa kuwa beki wa klabu ya Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' amesema hatoweza kamwe kuendelea kuichezea timu yake hata kama tatizo la uhaba wa fedha litaendelea kuiandama.

Beki huyo aliyeichezea Yanga kwa mafanikio na muda mrefu, ameeleza klabu hiyo imemtoa mbali zaidi hivyo ataendelea kuitumikia mpaka pale umri wake utakapokuwa umemshika mkono.

Kauli ya Cannavaro imekuja kufuatia baadhi ya wachezaji wa Yanga kuanzisha migomo baridi hivi karibuni kutokana na madai ya mishahara huku wengine wakiondoka na kuelekea mahala pengine.

Lakini Nahodha huyo wa muda mrefu, ameamua kufunga na kuelezea hisia zake ndani ya Yanga ambayo imemtoa mbali akisema hawezi kuiacha kwa namna yoyote ile.

Kikosi cha Yanga kipo katika maandalizi ya kikijiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia FC utakaopigwa Kenya Julai 18 2018 kwenye Uwanja wa Machakos jijini Nairobi.

1 COMMENTS:

  1. Canavaro unajuwa na unajijuwa vizuri kuwa umekwisha na hata pindi ukiamuwa kuingia mitini hakuna timu yeyote itayokuwa na hamu ya kukusajili kama ilivo kwa wengineo kama vile Kesi au Yondani na unstoa kauli hizo ili Yanga wakuonee huruma ubakie ule mshshara pale pindi Yanga wakiwanazo lakini zako zimekwisha na ukiondoka hapana atayevutiwa nawe na huku umekikosa chochote kutoka Yangs. Jee pale nawe ulipojiweka kando ulishaeishiwa na timu yeyote kama ilivo kwa Yondani?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic