July 1, 2018


Na George Mganga

Kikosi cha Gor Mahia kimeshindwa kulinda mabao yake mawili kwa kuufanya mchezo dhidi ya Gor Mahia umalizike kwa sare ya mabao 2-2 katika mashindano ya KAGAME.

Gor Mahia walikuwa wa kwanza kuandika mabao yao kupitia kwa Tuyisenge Jacques katika dakika ya 34 pamoja na Mieno Humphrey kwenye dakika ya 40 kipindi cha kwanza.

Rayon walionekana kubadilika zaidi kipindi cha pili kwa kugeuza kibao wakilishambulia lango la wapinzani wao kusaka mabao ya kusawazisha.

Alikuwa ni Ismailia Diarra alianza kucheka na nyavu za Gor Mahia mnamo dakika ya 62 kwa kuiandikia bao la kwanza.

Zikiwa zimesalia dakika mbili mpira kumalizika, Kwizera Pierre aliweza kuiandikia Rayon bao la pili na la kusawazisha mnamo dakika ya 88.

Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika timu zote mbili zilikuwa na mabao hayo mawili kwa mawili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic