CROUCH, MAGUIRE, GIROUD, WILLIAN, COURTOIS: TETESI KUBWA ZA SOKA ULAYA LEO JUMATATU
Burnley inatayarisha £500,000 kumnunua mshambuliaji wa Stoke Peter Crouch, mwenye umri wa miaka 37. (Sun)
Mlinzi wa England Harry Maguire, mwenye umri wa miaka 25, ana hamu ya kuhama kwa thamani ya £65m kwenda Manchester Unitedlakini hatolazimisha uhamisho , na Leicester inaona uzito kumuuza. (Mirror)
Jordan Pickford anatarajiwa kupewa mktaba mpya Everton wakati wanapotazamia kutathmini mustakabali wa kipa huyo wa England mwenye umri wa miaka 24- aliyehusishwa na uhamisho kwenda Chelsea. (The Times)
Real Madrid imewasilisha ombi la kwanza kwa Chelsea la thamani ya £100m kwa kipa Thibaut Courtois, mwenye umri wa miaka 26, na mchezaji wa kiungo cha kati Willian, aliye na miaka 29. (Mail)
Huenda Chelsea ikamuwania mlinzi wa Juventus Mattia Caldara, mwenye umri wa miaka 24, badala ya mshambuliaji Gonzalo Higuain, aliye na miaka 30, ambaye aliwahi kuhusishwa na uhamisho kwenda the Blues. (Corriere della Sera)
Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino ametupilia mbali shutuma za timu hiyo kumsajili upya Gareth Bale, kutoka Real Madrid, lakini amesema anatambua umuhimu wa kusajili wachezaji wapya. (Sky Sports)
Aston Villa wamewasilisha ombi la kumsajili mchezaji wa Liverpool Ben Woodburn kwa mkopo, huku mchezaji huyo wa miaka 18 kutoka Wales akitarajiwa kuondolewa kutoka kambi ya mazoezi ya kikosi cha Jurgen Klopp nchini Ufaransa (Telegraph)
Mshambuliaji wa Chelsea Olivier Giroud anapanga kuipigania nafasi yake Stamford Bridge, licha ya kufanya mazungumzo na Marseille. (Mail)
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho anasema hangenunua tiketi ya kutazama mechi ambapo timu yake ilifungwa 4-1 Liverpool katika ziara yao Marekani kabla ya kuanza kwa msimu. (Star)
Kutoka BBC
0 COMMENTS:
Post a Comment