July 30, 2018



Wakati kikosi cha Simba kikiwa katika programu ya mazoezi nchini Uturuki kwa takribani wiki moja sasa, kiungo mpya wa Yanga, Feisal Abdallah ‘Fei Toto’ ametoa somo kwa wachezaji wenzake jinsi ya kufanya ili waweze kuwapoteza Wekundu wa Msimbazi msimu ujao.

Kwa mujibu wa Championi, Toto ambaye amejiunga na Yanga hivi karibuni akitokea JKU ya Zanzibar ameliambia Championi Jumatatu kuwa, anaamini kuwa kama wachezaji wote wa Yanga watakuwa na hamu ya mafanikio anaamini watawapoteza Simba. Alisema usajili uliofanywa na Yanga ni mzuri na anaamini kuwa watafanya vizuri kama wote kwa pamoja watakuwa wanataka mafanikio bila kujali upungufu ambao upo.

“Watu wengi wanaiona Simba kuwa imefanya usajili mzuri lakini pia hata Yanga ina kikosi kizuri tena cha ushindani na chenye uwezo mkubwa wa kuipoteza kabisa Simba. “Hata hivyo, kama wachezaji wote tutashirikiana na kuwa na nia moja ya kutaka mafanikio naamini hakuna timu ya kutusumbua hata hao Simba.

“Ukiangalia uwezo na rekodi ya mchezaji mmojammoja kati yetu na hao wa Simba hatuzidiani sana kwa hiyo kama tutazingatia hayo, naamini tutafanya vizuri,” alisema Fei Toto.

4 COMMENTS:

  1. Mdomo kazi yake kuongea namuoeahuruma kama singano vile,mpekesi habari aumuite chemba akujuze ya jangwani,kama hapatikani muulize telela,fei karibu jangwani yajayo yanafurahishs

    ReplyDelete
  2. Kwanini mbinu hizo hukuwapa wenzako mlipocheza na timu ya Gor? au ndio unajaribu kupata imani uonekane mwenye ujuzi na mazoezi ya hali ya juu kuweza kumpiku Yondani? Polepole wewe bado mtoto mdogo

    ReplyDelete
  3. VPL unaijua dogo au ndo kulopoka tu
    Tulia na fanya kazi kwa bidii unapotaka utafika tu

    ReplyDelete
  4. Mtu mwenyewe unaitwa TOTO
    Kuna kitu kweli hapo!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic