July 2, 2018


Ukurasa wa Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, umerejeshwa tena Instagram baada ya kutekwa na watu wasiojulikana kwa takribani siku tatu zilizopita.

Haji ambaye amekuwa akiutumia ukurasa huo kwa ajili ya kuweka masuala yake binafsi pamoja na yanayoihusu klabu, ameurejesha ukurasa wake baada ya kusaidia na wataalamu wa teknolojia (IT).

Baada ya kufanikiwa kuurejesha, Manara amefunguka machache kwa kusema alikuwa katika wakati mgumu kufuatia wahuni kuvamia ukurasa wake huo wenye azidi ya wafuasi zaidi ya laki 3 na zaidi.


"Kuna siku ntasema, leo niwaambie neno moja tu, asanteni wote mlioguswa baada ya account yangu hii kutekwa, kiukweli nilikuwa totally confused" ameandika Manara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic