Mabingwa wa Kombe la Shirikisho la Azam Sports, Mtibwa Sugar, leo wamewatembelea watoto yatima wa kituo cha Vingunguti.
Mtibwa Sugar wameongozwa na Kocha wao, Zubery Katwila na viongozi wengine pamoja na wachezaji.
Mtibwa Sugar pia walibeba kombe la la ubingwa wa Shirikisho na kujumuika pamoja na watoto hao ikiwa ni sehemu ya faraja.
Hili ni jambo jema na Mtibwa Sugar wanapaswa kupongezwa kwa jambo hili zuri na wengine wakiweza wanaweza kuiga.
0 COMMENTS:
Post a Comment