Straika mpya wa klabu ya Simba, Meddie Kagere, amefanikiwa kucheka na nyavu kwa mara ya kwanza akiwa amevalia uzi mwekundu wa timu hiyo katika michuano ya KAGAME Cup dhidi ya APR ya Rwand.
Katika mchezo uliopigwa jana Uwanja wa Taifa, ulimalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 huku Kagere akifunga bao muhimu katika dakika za mwisho kabisa kuelekea kumalizika kwa mchezo.
Kagere alifunga bao hilo kwa mkwaju wa tuta zikiwa zimeongezwa dakika tatu pekee mechi iweze kumalizika, penati ambayo ilipatikana baada ya Kagere mwenyewe kuangushwa katika eneo la hatari.
Bao la Kagere limemuwezesha kuandika rekodi ya kufunga bao la kwanza kwenye mchezo wake wa kwanza akiwa na jezi ya Simba na akifanikiwa kucheza dakika 90 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
HIVI HUWA HAUNA CHA KUANDIKA? KUBWA J, MPUUZI KABISA
ReplyDeleteWatapata tabu sana
ReplyDelete