July 7, 2018


Wakati dirisha la usajili kwa klabu za Ligi Kuu Bara likiwa wazi, uongozi wa Singida United umefanikisha kunasa saini ya miaka mitatu kutoka kwa aliyekuwa kipa wa Simba, Davd Kisu.

Kipa huyo amefikia maamuzi hayo na mabosi wa Singida United ili kuwa sehemu ya kikosi chao kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Bara kumpa tafu Manyika Jr pamoja na Ally Mustapha 'Barthez'.


Kisu alikuwa mlinda mlango ndani ya kikosi cha Njombe Mji ambayo ilishuka daraja katika msimu uliomalizika (2017/18) ikiwa mkiani kwa kujikusanyia alama 22 pekee.

Imeelezwa Kisu alikuwa na timu ya Singida kambini huko Mlandizi wakati kinaweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya KAGAME lakini hakuweza kusaini ili kukamilisha baadhi ya mambo yaliyokuwa hayajakaa sawa.

Lakini baadaye baada ya mambo kwenda sawa, Kisu alifikia mwafaka na Singida kisha kusaini mkataba huo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic