KIPIGO KUTOKA GOR MAHIA CHAWAFANYA YANGA KUITUPIA LAWAMA TFF, SABABU NI HIZI
Baada ya kuambulia kichapo kingine cha mabao 3-2 dhidi ya Gor Mahia FC katika mchezo wa mkondo wa pili wa Kombe la Shirikisho Afrika, uongozi wa Yanga umeibuka na kuitupia lawama TFF.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika, ameibuka na kusema TFF imesababisha Yanga kuambulia kichapo hicho kutokana na kuwachukua nyota wake watano kwa ajili ya masuala ya kitaifa.
Nyika ameeleza TFF iliwaita wachezaji hao akiwemo Ibrahim Ajibu kwa lengo la kupiga picha na mwisho wa siku kuwarejesha kambini muda ukiwa umeenda kitu ambacho anaamini kimeweza kusababisha Yanga kupoteza.
Kiongozi huyo amesema wachezaji hao walichukuliwa majira ya mchana na kurudi kambini mida ya saa moja kuelekea saa mbili akieleza kuwa ni kitu ambacho kimepelekea wapatwe na uchovu.
Baada ya kichapo hicho, Yanga sasa imeendelea kushikilia mkia kunako kundi D kwa kujikusanyia alama moja pekee huku MC Alger wakiwa kileleni na Gor Mahia wakikamata nafasi ya pili na Rayon Sports ikishika namba 3.
Viongozi wa Yanga akili hamna kabisa ...kwani yanga wapo chezaji wawili tu..acheni umama memezowea kubebwa bebwa sasa hivi mnapitia haki mnalia lia kima wanawake sasa hapo TFF inaingiliana vipi..????
ReplyDeleteKuna haki gani wewe acha ushabiki ......
DeleteManeno ya kupotosha. Si ajabu kushindwa kila mtu akiyataraji hayo. Wamechukuliwa wamekwenda kufanywa nini?
ReplyDeleteHayo maneno ya mkosaji haya mechi ya kwanza mbona tumefungwa 4 wachezaji nao walichukuliwa na tff tuseme ukweli tu hawawezi gor mahya
ReplyDelete