July 31, 2018


Wakati kikosi cha Simba kikiendelea kujifua vilivyo huko nchini Uturuki kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara, kocha mkuu wa timu hiyo raia wa Ubelgiji, Patrick Aussems amewapa mtihani mzito washambuliaji wa timu hiyo akitaka mabao mara mbili ya yale ya msimu uliopita.

Aussems ambaye amejiunga na Simba hivi karibuni akichukua mikoba ya Mfaransa, Pierre Lechantre amewataka washambuliaji timu hiyo kuhakikisha msimu ujao wanaongoza timu hiyo kufunga mabao mengi zaidi ya yale waliyofunga msimu uliopita.

Katika msimu uliopita Simba ilifanikiwa kufunga mabao 62 katika mechi 30 ilizocheza kwa hiyo kutokana na maagizo hayo ya Aussems kwa washambuliaji hao watatakiwa kufunga zaidi ya mabao 120 msimu ujao ambayo ni mara mbili zaidi ya yale ya msimu uliopita lakini sasa wakiwa wanatakiwa kucheza michezo 38. 

Kwa mujibu wa Championi, Mohamed Rashid alisema kuwa kocha huyo ameļ¬kia hatua hiyo kutokana na mazoezi ya uhakika ya kuzifuma- nia nyavu ambayo ame- kuwa akiwapa- tia washambu- liaji wa timu hiyo.

CHANZO: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic