July 31, 2018


Uongozi wa klabu ya Simba umefunguka na kusema kuwa haushinikizwi kufanya uchaguzi wake na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) zikiwa zimesalia siku kadhaa kuelekea mchakato wake kuanza.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, amesema wao kama Simba walikuwa wanasubiria katiba yao mpya isajiliwa na serikali hivyo mchakato wa uchaguzi ulisimama kwa muda kuisubiria.

Manara ameeleza kuwa wao kama Simba hawawezi kushinikiwa kufanya uchaguzi huo na TFF na badala yake watakutana Agosti 31 kuanza mchakato kamili wa kuunda Kamati ya Uchaguzi.

Hivi karibuni, Rais wa TFF, Wallace Karia aliwapa Simba siku 75 kwa ajili ya kuanza mchakato huo baada ya kupokea barua inayoeleza kuwa klabu hiyo inapaswa kufanya uchaguzi mwingine baada ya viongozi waliopo madarakani kumaliza muda wao.

Simba imekuwa ikiongozwa na Kaimu Rais, Salim Abdallah 'Try Again' ambaye amekaimu nafasi hiyo kutoka kwa Evans Aveva mbaye yuko mahakamani kutokana na makosa ya matumizi mabaya ya fedha.


2 COMMENTS:

  1. Haibiidi kutoa kauli hiyo ya siku 75 Ne akijuwa vizuri kuwa mambo yalikuwa kwao TFF kuymaliza. Hii ni kama msimamizi wa miyihani shuleni akiwaonya wanafunzi wamalize mitihani kwa muda wa saa mbili wakati msimamizi huyo hajagawa hiyo mitihani kwa wanafunzi

    ReplyDelete
  2. hao viongozi wanapochaguliwa wanajua muda wao unamalizika lini acheni kutengeneza migogoro mingine isiyo na faida huu wa yanga chanzo chake ni hichohicho itisheni uchaguzi sasa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic