KOCHA AZAM ATAKA KUWAFANYA UMAFIA HUU KWA TIMU ZA LIGI BAADA YA KAMBI UGANDA
Wakati leo Jumatatu kikosi cha Azam FC kikitarajia kukwea pipa na kuelekea nchini Uganda kwa ajili ya kambi yake ya muda mfupi, kocha mkuu wa timu hiyo, Mholanzi Hans van Der Pluijm ameweka bayana kuwa watakapotoka nchini humo kikosi chake kitakuwa tayari kwa ajili ya mapambano ya ligi kuu kwa msimu ujao.
Azam FC ambao ni mabingwa wa Kombe la Kagame, leo Jumatatu itakuwa timu ya pili kwenda kuweka kambi nje ya nchi baada ya Simba ambao wenyewe wapo Uturuki kwa wiki sasa.
“Tunaenda Uganda lakini jambo kubwa ambalo ninalitazamia ni kwamba tutatumia vizuri safari ya huko kwa ajili ya kuzidi kukiboresha kikosi chetu baada ya kumalizika kwa Kombe la Kagame ambapo hatukuwa na wachezaji wote kama ilivyo sasa.
“Tunaamini kwamba tukiwa huko tutatumia mbinu zote ili kukifanya kikosi kiwe na makali zaidi ili hata tutakapokuja kwenye ligi tuwe na nguvu ya kupambana na wapinzani wetu, kujiandaa na michezo ya kirafiki tutakayocheza itatusaidia kwa kiwango kikubwa zaidi,” alisema Mholanzi huyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment