July 5, 2018



Kama mambo yatakwenda sawa, Kocha Patrick Aussems atasaini mkataba leo kuanza kuinoa Simba.

Aussems raia wa Ubelgiji tayari yuko nchini akiendelea na mazungumzo na Simba.

Jana alikuwa uwanjani kuishuhudia Simba ikiivaa Singida United katika mechi ya michuano ya Kombe la Kagame.

"Kweli kocha yuko nchini na kama mambo yatakwenda vizuri basi atasaini kati ya leo au kesho. Tayari ameiona timu ikicheza dhidi ya Singida United. Amekuwa na maoni yake ingawa hajazungumza sana," kilieleza chanzo.



Aussems mwenye umri wa miaka 51 ni kati ya makocha waliowahi kuzinoa timu mbalimbali za Afrika.

AC Leopards ya Congo, ni moja ya timu ambazo alifanya nazo vizuri kama ilivyokuwa kwa KSA Yaounde ya Cameroon.

Kabla aliwa kuwa kocha msaidizi nchini Ufaransa ambako alizinoa timu za Reims na SCO Angers lakini akafanikiwa kuwa kocha mkuu akiinoa Stade Beaucairois ya Ufaransa pia.

7 COMMENTS:

  1. UKIANDIKA HABARI ZA TIMU YAKO AKILI HUWA INAKURUDIA, SI NDIO!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yanga mtapata tabu sana..maana hata taarifa haiwahusu..ila mnajishtukia mnasemwa nyie.. na bado mnyama ataendelea kuwatesa sanaa

      Delete
  2. THIS IS BONGO! Tumebadili Akili kubwa kwa Akili ndogo, kisa Maslahi! Huwezi kupata pepo bila kufa! LET US SEE!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kipindi cha mpito huwa na majaribio mengi. Tusiongee sana na kulaumu kila hatua, atapatikana mtu sahihi muda ukifika. Uwepo wa Masoud Djuma kikosini unasaidia kujenga uti wa mgongo wa team. Hapa Masoud anaandaliwa kuwa kocha mkuu so experience kutoka kwa walio juu ki uwezo inamjenga. Akili kibwa unaemtaja ametaka pesa nyingi ambayo kwa sasa club isingeweza kubeba hiyo risk. Tatizo letu tunataka mafanikio ya haraka bila kuangalia uwezo

      Delete
  3. Mpeni muda kocha wabongo hatuchelewi kuleta uswahili halafu naye akaonyeshwa mlango wa kutokea

    ReplyDelete
  4. KWAHIYO SIMBA ITAKUWA NA WABELGIJI WAWILI, MANARA NA HUYO ALIYE KUJA SASA, HONGERA KAMA WABELGILI NDIO SULUHISHO LA UJINGA WENU!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic