July 5, 2018


Wakati michuano ya Kombe la Dunia ikiendelea nchini Urusi, pweza aliyekuwa anaaminika katika kubashiri matokeo ya mechi kadhaa zilizopita zikiwemo za timu ya taifa ya Japan,  ameuawa na kugeuzwa kiteweo.

Pweza huyo aliyekuwa akifahamika kwa jina la Rabio amejizolea umaarufu mkubwa kwenye michuano hiyo kutokana na umahiri wake katika kubashiri mshindi wa mechi husika.

Mmiliki wa pweza huyo ambaye ni mvuvi anayetambulika kwa jina la Lakini Kimio Abe amesema kuwa ameamua kumuuza na kugeuzwa kitoweo kwa kuwa amebaini atajizolea kitita kikubwa  cha fedha kuliko kama angeendelea na utabiri ambao haujamnufaisha licha ya kupatia.

Rabio ambaye alikuwa pweza mkubwa,  amefanikiwa kuibashiria Japan kupata kipigo dhidi ya Colombia na hata sare yao dhidi ya miamba ya soka ya Afrika timu ya taifa ya Senegal.

Baada ya kuibashiria Japan kufungwa dhidi ya Ubelgiji hatua ya 16 bora, Rabio hakuweza kushuhudia utabiri wake ukitimia kutokana na kuingizwa sokoni.

Abe amesema yupo pweza mwingine atakayeendelea kubashiri michuano hiyo nchini Urusi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic