July 3, 2018


Na George Mganga

Beki wa kimataifa katika klabu ya Simba, Asante Kwasi, amerejea nchini kutoka Ghana na kuanza mazoezi kwenye fukwe za Coco zilizopo jijini Dar es Salaam.

Kwasi amewahi kurudi Tanzania na kuanza mazoezi yake binafsi kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Beki huyo aliyesajiliwa na Simba kutokea Lipuli FC ya Iringa, aliondoka nchini siku kadhaa baada ya ugawajwi wa tuzo za Mo kumalizika na kuelekea kwao Ghana kwa ajili ya mapumziko.

Ikumbukwe Kwasi hajajumuishwa kwenye kikosi cha Simba ambacho kinashiriki mashindano ya KAGAME hivi sasa akiungana na wachezaji wengine akiwemo James Kotei kutoka Ghana pia.

Wakati huo wachezaji wote kikosi cha Simba wanatarajiwa kuwasili kambini mwishoni mwa mwezi huu tayari kwa maandalizi ya msimu ujao na tamasha la Simba Day ambalo hufanyika Agosti 8 kila mwaka.



1 COMMENTS:

  1. Kwanini hatuwaoni akina Ndemla na vijana wa Tanzania kama akina Mohamed Husein, Mohamedi Ibrahim mo na wengine wengi wakihangaika kujiweka fiti? Au wana wanasubiri kuja kulialia kuwa wanawekwa benchi?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic