July 31, 2018


Kufuatia kipigo cha mabao 3-2 walichokipata Yanga juzi dhidi ya Gor Mahia FC, kipa wa zamani wa timu hiyo, Manyika Peter, amewataja wachezaji wake bora wawili ambao anaamini walipambana.

Kipa huyo amewataja mlinda mlango Youthe Rostand na kiungo Papy Kambamba Tshishimbi ndiyo waliokuwa na viwango vizuri huku wengine wote waliosalia akiwapa alama sufuri.

Kwa mujibu wa Radio One, Manyika amesema kwa namna ambavyo wachezaji hao walivyopambana kukipiga na Gor Mahia wanastahili pongezi kutokana na mechi hiyo kuwa ngumu.

Licha ya kukubali kichapo hicho, Manyika amesema Rostand alifanya kazi kubwa langoni huku Tshishimbi akipiga kazi nzito eneo la kiungo japo akikosa watu wa kuwatengenezea mipira ambayo ilikuwa inashindwa kutimiziwa majukumu.

Mbali na wachezaji hao bora, Manyika amesema Yanga inapaswa kufanya usajili wa maana kulingana na ukubwa wa klabu hiyo kuliko wachezaji wengi ilionao hivi sasa kwani hawaendani sawa na timu hiyo.

5 COMMENTS:

  1. MIMI SIYO MTABIRI ILA NI MCHAMBUZI WA HALI YA SOKA NCHINI. HAYA MATOKEO NILIYATARAJIA SIKU NYINGI TU NA NIKASEMA KUNA HUJUMA KUANZIA VIONGOZI WA KAMATI YA USAJILI NA MASHINDANO YA YANGA, BENCHI LA UFUNDI NA MTANDAO MKUBWA SANA AMBAO WENYE AKILI WANAUJUA. SASA USHAURI NI KWAMBA VIONGOZI,WALIOSALIA WANAOHUSIKA NA USAJILI WAONDOKE, BENCHI LOTE LA UFUNDI LIVUNJWE......ATAFUTWE KOCHA MPYA WA MUDA. KUNA MAKOSA YA KIUFUNDI NA WACHEZAJI KUATHIRIKA KISAIKOLOJIA, ANATAKIWA MTAALAMU WA SAIKOLOJIA....MORALI YA WACHEZAJI, IKIWAMO PESA, KUZIBA MAPENGO YA NAFASI YA BEKI WA KULIA, KATI NA WASHAMBULIAJI NAMBA 9, 10.....LAKINI HAYA MATOKEO NDIYO HALI HALISI YA UBOVU WA KIKOSI KILICHOSAJILIWA.......WAHUSIKA WANATAKIWA KUBEBA LAWAMA HIZI HAZIEPUKIKI

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kiongozi hizo ni dalili za wazi za ujauzito na ndizo zikufanyazo upest utumbo unaofanana kwenye kila hoja ilwtwayo hapa.

      Delete
    2. Kwanza andika kwa helufi ndogo.kuandika kwa helufi kubwa ni saws na kuongea kwa sauti kubwa wakati hamna umuhimu wowote. Pili kila habari inayoandikwa were unacopy huu ujumbe wako na kuubandika hapo.huu ujumbe wako hauendani ni kila habari humu ndani.

      Delete
    3. Acheni umama nyie..mkipewa tathimini za ukweli unaleta ushabiki mandazi...sasa hapo kitu gani hakiendani na hiyo habari mbona mna kuwa na akili mgando.?kiukweli benchi la ufundi lipigwe chini sasa hivi kabla ya league kuanza.

      Delete
  2. Huyu ndg yetu siyo mwungwana hata tumemshauri sana na huo ujumbe wake anaotaka kutuaminisha

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic