July 31, 2018


Real Madrid haina mpango wa kumsajili mchezaji wa safu ya kati wa Chelsea Willian, mwenye umri wa miaka 29, na wanaemtaka tu ni mlinda lango wa Ubelgiji Thibaut Courtois, mwenye umri wa miaka 26, kutoka the Blues. (Marca)

Mchezaji wa kimataifa wa Brazil Willian anasema ni mwenye ''furaha sana katika Chelsea na anafurahia kuishi London. (Globo Esporte, via Mirror)

Meneja wa Leicester Claude Puel amesisitizia tena imani yake kwamba mlinzi wa England Harry Maguire mwenye umri wa miaka 25 - anayechezea Manchester United - atasalia na the Foxes katika msimu mpya. (Sky Sports)

Maguire anatarajiwa kupewa donge nono katika mkataba wake mpya na Leicester na hivyo kuongezewa malipo yake ya wiki kutoka £50,000 hadi £95,000. (Mirror)

Everton wako mstari wa mbele katika harakati za kusaini mkataba na Mchezaji wa safu ya mashambulizi wa Manchester United na Argentina Marcos Rojo, mwenye umri wa miaka 28 ambae aliambiwa anaweza kuondoka kama tahamani yake ya £30m itatimizwa. (Mirror)

Liverpool wanajiamini kuwa wao ndio watakao saini mkataba na mshambuliaji wa Senegal Sadio Mane, mwenye umri wa miaka 26, kwa mkataba wa muda mrefu mnamo wiki zijazo. (Mirror)


Wakati huo huo , mchezaji wa the Reds kutoka Ubelgiji Divock Origi, 23, anasakwa kwa deni na Besiktas pamoja na Fenerbahce.(Talksport)

Kutoka BBC

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic