July 31, 2018


Baada ya Mcameroon, Youthe Rostand kupokea lawama nyingi kutoka kwa baadhi ya wanachama na mashabiki wa Yanga juu ya ubora wake golini, kipa wa zamani wa Yanga, Manyika Peter, ameibuka na kumtetea.

Manyika amesema kitendo cha mashabiki wengi wa Yanga kumtupia lawama Rostand hakina maana yoyote kutokana na kipa huyo kuonesha ubora stahiki uwanjani.

Manyika ameeleza anaamini Rostand ni kipa bora hivyo wale wote wanaomkosoa hawako sahihi na badala yake wazidi kumvunja nguvu za kuendelea kuitendea haki nafasi yake kwenye goli.

Kipa huyo ambaye aliwahi kutamba na Yanga miaka ya nyuma amewatupia lawama mabeki wa Yanga kutokana na kiwango walichoonesha akisema walisababisha Rostand kufungwa na si yeye kufanya makosa.

Manyika amesema mabeki wa Yanga na kikiso kizima kwa ujumla kiliwa na mapungufu mengi kitu ambacho kimepelekea timu kufungwa mechi mbili mfululizo huku akieleza mfumo ambao ulikuwa unatumika ulikuwa haueleweki.

Kufungwa kwa Yanga juzi na Gor Mahia kwa mabao 3-2 kumewafanya waendelee kuwa mkiani kunako kundi D wakiwa na alama moja pekee ambayo waliipata baada ya suluhu ya 0-0 dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda.

5 COMMENTS:

  1. MIMI SIYO MTABIRI ILA NI MCHAMBUZI WA HALI YA SOKA NCHINI. HAYA MATOKEO NILIYATARAJIA SIKU NYINGI TU NA NIKASEMA KUNA HUJUMA KUANZIA VIONGOZI WA KAMATI YA USAJILI NA MASHINDANO YA YANGA, BENCHI LA UFUNDI NA MTANDAO MKUBWA SANA AMBAO WENYE AKILI WANAUJUA. SASA USHAURI NI KWAMBA VIONGOZI,WALIOSALIA WANAOHUSIKA NA USAJILI WAONDOKE, BENCHI LOTE LA UFUNDI LIVUNJWE......ATAFUTWE KOCHA MPYA WA MUDA. KUNA MAKOSA YA KIUFUNDI NA WACHEZAJI KUATHIRIKA KISAIKOLOJIA, ANATAKIWA MTAALAMU WA SAIKOLOJIA....MORALI YA WACHEZAJI, IKIWAMO PESA, KUZIBA MAPENGO YA NAFASI YA BEKI WA KULIA, KATI NA WASHAMBULIAJI NAMBA 9, 10.....LAKINI HAYA MATOKEO NDIYO HALI HALISI YA UBOVU WA KIKOSI KILICHOSAJILIWA.......WAHUSIKA WANATAKIWA KUBEBA LAWAMA HIZI HAZIEPUKIKI

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ila wewe jamaa una dalili flani za Ufala,haiwezekani kila hoja iletwayo jukwaani hapa upest utumbo wako ulioutunga tangu wiki iliyopita

      Delete
    2. Yani huyo lazima mimba atakua nayo tu si bure comments zake utumbo tu humu

      Delete
    3. Ukweli mchungu..Lakini chungu mara zote ni dawa..
      Tulieni jama mpewe dozi juu ya vidonda vyenu!

      Delete
  2. Waache kulialia wasaidie klabu kulipa mishahara

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic