July 30, 2018


Baadhi ya mashabiki wa Yanga wameendelea kulia na uongozi wao juu ya kipa Youthe Rostand kutokana na kiwango chake ikiwa ni baada ya timu hiyo kupoteza mchezo wa Kombe la Shirikisho kwa mabao 2-3 dhidi ya Gor Mahia FC.

Yanga ilipoteza mechi hiyo jana huku lawama nyingi zikienda kwa mlinda mlango, Mcameroon, Rostand ambaye aliruhusu nyavu zake kuguswa mara tatu.

Mashabiki hao wamesema ifikie wakati kama vioongozi wajua namna wao kama mashabiki wanavyoumia pindi timu hiyo inapopoteza uwanjani kutokana na ukubwa wa jina lake pamoja na ukongwe ilionao.

Wengi wao wamezidi kuchukizwa na uongozi juu ya kipa huyo kuendelea kukaa langoni ilihali kila siku wamekuwa wakipiga kelele za kuutaka uwape nafasi makipa wengine ikiwemo Beno Kalomabya ambaye muda mwingi amekuwa hachezi.

Aidha, kupitia mitandao ya kijamii, wengi wameelezea masikitiko yao kutokana na namna pia kikosi chao kinavyocheza wakiomba nguvu iongezwe ndani ya Yanga ili kuifanya timu hiyo iweze kurudi kama zamani ilivyokuwa.

10 COMMENTS:

  1. MIMI SIYO MTABIRI ILA NI MCHAMBUZI WA HALI YA SOKA NCHINI. HAYA MATOKEO NILIYATARAJIA SIKU NYINGI TU NA NIKASEMA KUNA HUJUMA KUANZIA VIONGOZI WA KAMATI YA USAJILI NA MASHINDANO YA YANGA, BENCHI LA UFUNDI NA MTANDAO MKUBWA SANA AMBAO WENYE AKILI WANAUJUA. SASA USHAURI NI KWAMBA VIONGOZI,WALIOSALIA WANAOHUSIKA NA USAJILI WAONDOKE, BENCHI LOTE LA UFUNDI LIVUNJWE......ATAFUTWE KOCHA MPYA WA MUDA. KUNA MAKOSA YA KIUFUNDI NA WACHEZAJI KUATHIRIKA KISAIKOLOJIA, ANATAKIWA MTAALAMU WA SAIKOLOJIA....MORALI YA WACHEZAJI, IKIWAMO PESA, KUZIBA MAPENGO YA NAFASI YA BEKI WA KULIA, KATI NA WASHAMBULIAJI NAMBA 9, 10.....LAKINI HAYA MATOKEO NDIYO HALI HALISI YA UBOVU WA KIKOSI KILICHOSAJILIWA.......WAHUSIKA WANATAKIWA KUBEBA LAWAMA HIZI HAZIEPUKIKI

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sasa morali ya wachezaji itatoka wapi na umeshaambiwa pesa hakuna

      Delete
  2. Ajabu kubwa ni kua TV ya Azam mpaka mwisho wa mchezo ilionesha yanga ikiongoza kwa bao moja lililoingia kipundi cga kwanza kwa njia ya kona. Kwahakika ni msiba si mdoko

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ulikuwa unaangalia Yanga wakicheza na Ndanda kijana. Mechi ilikuwa ZBC2 pekee. Pole. Yaaani umekomaa na Ndanda vs Yanga mpaka Mrisho ukijua unaangalia Yanga vs Gor Mahia ������

      Delete
    2. May be alivutiwa kuona wanaongoza akaona hiyo ndiyo yenyewe

      Delete
    3. Nimecheka sana watu wanaangalia live kumbe wengine wanaangalia Recorded

      Delete
  3. Katika kombe la Kagame yanga walifurahi sana pale simba walipofungwa na Azam lakini jana nimewashuhudia wanasimba wakiweka nyuso chini kuihurumia yanga. Hilo inabidi liwe somo kwa yanga

    ReplyDelete
  4. Youth Rostand jana pamoja na mistake zake kidogo, lakini kaokoa sana. Jana kwa maoni yangu beki line nzima ndio ilikuwa mbovu. Na yanga kusema ukweli namba 2 itakuwa shida mwaka huu. Timu ikitulia wachezaji wote wakafanya mazoezi ya nguvu , itatoa ushindani sana.

    ReplyDelete
    Replies
    1. huenda ni wachache aa wataliona hili, nilihesabu bao nne za wazi alizookoa, ushabiki wa mhemuko

      Delete
  5. Sijawahi ona blog ambayo haina ukamilifu Wa habari kama hii. Nilikua namheshimu mno Saleh Ally kua ni mkongwe na anajua kukidhi hamu ya wasomaji. Kinachofanyika hapa ni wizi Wa macho macho. Anaandika kichwa cha habari kukuvuta kumbe hakuna lolote. Umeliwa kqa kumaliza ka vocha kako yeye tayari kaingiza pesa. Aibu sana Saleh jembe, weka habari ijitosheleze

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic