Baada ya kuambulia kichapo cha mabao 3-2 jana katika mchezo wa mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kkikosi cha Yanga kimeweka rekodi ya kucheza dakika 360 bila kupata alama tatu.
Yanga imepoteza mechi hiyo ya mkondo wa pili kwa mabao yaliyofungwa kimiani na George Odhiambo, Jacques Tuyisenge na Haron Shakava kwa upande wa Gor Mahia.
Kwa upande wa Yanga, mabao yamefungwa na kiungo mshambuliaji Deus Kaseke ambaye alisajiliwa kutoka Singida United pamoja na Raphael Daudi.
Yanga imeshindwa kupata alama hizo kutokana na kupata suluhu moja pekee kunako kundi D dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda na ikipoteza mechi mbili ilizofungwa na Gor Mahia pamoja na moja dhidi ya MC Alger.
Yanga imeshikilia mkia ikiwa na alama 1 ambayo iliipata baada ya matokeo ya 0-0 katik amchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam dhidi ya Rayon na kujiweka katika nafasi ya 4.
Baada ya mechi hiyo, msimamo sasa unaonesha timu zote zimecheza mechi 4 huku MC Alger ikiwa kileleni na alama 8 ikiizidi Gor Mahia kwa tofauti ya mabao ya kufungwa na kufunga huku Rayon ikishika namba tatu na Yanga ikiwa mwishoni.
MIMI SIYO MTABIRI ILA NI MCHAMBUZI WA HALI YA SOKA NCHINI. HAYA MATOKEO NILIYATARAJIA SIKU NYINGI TU NA NIKASEMA KUNA HUJUMA KUANZIA VIONGOZI WA KAMATI YA USAJILI NA MASHINDANO YA YANGA, BENCHI LA UFUNDI NA MTANDAO MKUBWA SANA AMBAO WENYE AKILI WANAUJUA. SASA USHAURI NI KWAMBA VIONGOZI,WALIOSALIA WANAOHUSIKA NA USAJILI WAONDOKE, BENCHI LOTE LA UFUNDI LIVUNJWE......ATAFUTWE KOCHA MPYA WA MUDA. KUNA MAKOSA YA KIUFUNDI NA WACHEZAJI KUATHIRIKA KISAIKOLOJIA, ANATAKIWA MTAALAMU WA SAIKOLOJIA....MORALI YA WACHEZAJI, IKIWAMO PESA, KUZIBA MAPENGO YA NAFASI YA BEKI WA KULIA, KATI NA WASHAMBULIAJI NAMBA 9, 10.....LAKINI HAYA MATOKEO NDIYO HALI HALISI YA UBOVU WA KIKOSI KILICHOSAJILIWA.......WAHUSIKA WANATAKIWA KUBEBA LAWAMA HIZI HAZIEPUKIKI
ReplyDelete