July 6, 2018


Mshambuliaji Mbwana Samatta yuko nchini Uholanzi ambako timu yake ya KRC Genk, imeweka kambi.

Genk imesafiri kutoka Ubelgiji hadi nchi jirani ya Uholanzi kwa ajili ya kambi hiyo.

Kikosi cha Genk kimeendelea na kujifua kwa ajili ya kujiweka sawa kabla ya kuanza msimu mpya.

Samatta ambaye pia ni nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ni kati ya wachezaji wanaoendelea kujifua katika kikosi hicho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV