MINZIRO ASAINI MWAKA MMOJA ARUSHA UNITED ILI KUIPANDISHA LIGI KUU
Aliyekuwa Kocha Mkuu wa klabu ya KMC ya Kinondoni, Dar es Salaam, Fred Felix Minziro, amechaguliwa kuifundisha timu ya Arusha United kwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja.
Minziro ambaye aliwahi kuzipandisha daraja mpaka Ligi Kuu klabu za Singida United na baadaye KMC, ameingia kwenye kibarua kingine cha kuipigania Arusha United ipande daraja pia.
Kocha huyo ameingia kandarasi hiyo ya mwaka mmoja ikiwa ni siku chache zimepita baada ya aliyekuwa Ofisa Mtendaji Azam, Saad Kawemba kuchaguliwa kuwa CEO kwenye klabu hiyo iliyojulikana kwa jina la JKT Oljoro.
Arusha United hivi sasa ipo Ligi Daraja la Kwanza na sasa itakuwa inapambana kwa ajili ya kujipatia nafasi ya kushiriki Ligi Kuu Bara msimu wa 2019/20 endapo itafanikiwa kupanda daraja.
0 COMMENTS:
Post a Comment