July 4, 2018


Uongozi wa klabu ya SIngida United umesema kuwa bado haujapokea barua rasmi kutoka Yanga ikimtaka mchezaji wake, kiungo Deus Kaseke.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya tetezi zilizokuja kwa kasi kuwa mabosi wa Yanga tayari wameshamalizana na mchezaji huyo waliyewahi kuwa naye.

Mkurungenzi wa klabu hiyo, Festo Sanga, amesema Yanga bado hawajatuma barua kumuhitaji mchezaji huyo ambaye ameonesha nia ya kurejea Yanga.

Sanga amesema kama Yanga wataamua kufuata taratibu zote stahiki za usajili hawatoweza kumzuia kwa sababu hata mchezaji mwenyewe anaihitaji Yanga.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Kamati ya usajili Yanga, Hussein Nyika, alisema juzi kuwa suala la mchezaji huyo kusajiliwa lipo chini ya benchi la ufundi na kama atasajiliwa wataliweka wazi baadaye.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic