July 4, 2018



Kama ulikuwa hujui sikukuu ya sabasaba hii (7/7) uende kiwanja gani kula bata jibu lake utalipata ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar ambapo wakali kibao wakiongozwa na Barakah The Prince na Young Dee watapanda na kukamua shoo ba’b kubwa inayotambulika kwa jina la Usiku wa Washkaji.

Akizungumza na Risasi Vibes, Meneja na Mratibu wa Dar Live, Rajabu Mteta ‘KP Mjomba’ alisema kuwa, shoo hiyo ni maalumu kwa washkaji na imetokana na ‘tour’ ya Kuvichaka’ ambayo huandaliwa na Mtangazaji wa Ladha 360, Jabir Saleh.

“Utakuwa ni Usiku wa Washkaji kweli, mbali na Young Dee na Baraka The Prince, wakali wengine tutakaokuwa nao ni Zaiid mzee wa Wowowo, Country Wize au Country Boy, Moni wa Centrozone huku kwenye Singeli kukiwa na wakali kibao kama vile Yuda Msaliti na Virus,” alisema KP Mjomba. Kiingilio katika usiku huo kitakuwa shilingi 5,000 tu getini.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic