July 4, 2018


Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera, amefurahishwa na kiwango cha Mrisho Ngassa ambaye amerejea katika timu hiyo.

Kwa mujibu wa Meneja wa kikosi cha Yanga, Hafidh Saleh, amefunguka na kusema kuwa Zahera amefurahishwa na mwenendo wa mchezaji huyo ambaye alikuwa akiichezea Ndanda FC msimu uliopita.

Saleh ameeleza kuwa Zahera amemuona Ngassa kuwa bado ana uwezo licha ya kuelezwa kuwa hataweza kuendana na kasi ya Yanga kutokana na kutoichezea kwa muda mrefu.

Wachezaji wa Yanga chini ya Mkongo huyo kimeendelea na mazoezi yake jana kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Gor Mahia FC.

Yanga watakuwa na kibarua hicho Julai 18 2018 kwenye Uwanja wa Manchakos jijini Nairobi kabla ya kurudiana tena hapo baadaye jijini Dar.

5 COMMENTS:

  1. Ngassa naona atapata tabu sana kwenye ligi maana uwezo wake umeshaisha

    ReplyDelete
  2. Yanga inajipa Moyo.halafu Tarimba anasema wana mascout wa Uhakika.sasa inakuwaje unaleta rundo la wachezaji kufanya majaribio ?

    ReplyDelete
  3. Namba 5, 6, 9, 7, 11 na 10 ndio nafasi za kuzibwa

    ReplyDelete
    Replies
    1. 5,8,9,11,10. Namba 6 yupo Tshishimbi. Tatizo tumembadilishia majukumu

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic