Baada ya kuleta takribani wachezaji 14 kutoka nje ya nchi waliokuja kufanya majaribio na kikosi cha Yanga nchini, jumla ya 8 wameondoka na 6 wakibakia.
Meneja Mkuu wa timu, Hafidh Saleh, amesema kwa sasa wamebaki na wachezaji 6 pekee huku wengine wakifeli mazoezi ambapo sasa watakuwa wanarejea makwao.
Saleh amesema wachezaji waliofeli wameondoka kutokana na mchujo unaoendelea kwa ajili ya kupata wale wanaohitajika kwa ajili ya kukisuka upya kikosi.
Ikumbukwe siku kadhaa zilizopita, Yanga ilitanga kuleta wachezaji 14 wa kimataifa kwa mujibu wa Ofisa Habari wa klabu, Dismas Ten kwa ajili ya kufanya majaribio.
Kikosi hicho kipo kambini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia FC ya Kenya na msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.
Hivi huu mfumo wa kuita wachezaji kuja kufanya majaribio ndipo wasajiliwe ni ule ambao scout analeta cv ya mchazaji na kocha anahitaji kumuona? Au yeyote tu anajitokeza pale kujaribu bahati yake. Msaada wadau cjaelewa.
ReplyDeleteNi wa mascout kuleta CV then wanafanya majaribio
DeleteTunataka Kikosi Kazi Viongozi Wampe Kocha Nafasi Afanye Kazi.
ReplyDeleteYanga ndio timu pekee tanzania yenye scouting kwa mujibu wa tarimba
ReplyDeleteWakifanya wengine mnaliita bonanza. Hahaaaa njaa haimuachi mtu. Lini yanga ikafanya majaribio anzia kina niyonzima, ngoma, chirwa nawengine. Kweli weka akiba ya maneno.
DeleteSana chama langu kubwa YANGA. Siye tupo Nyuma yenu
ReplyDeleteHahaa,si mlisema nyie mna wataalam(scouts).Sasa inakuaje wataalam wanaleta wachezaji wabovu?Mtapata taabu sana
ReplyDeleteOhh
ReplyDelete