July 1, 2018


Michuano ya Kombe la Dunia inaendelea tena leo kwa mechi mbili kuchezwa huko Russia baada ya Ufaransa na Uruguay kufuzu jana kuingia hatua ya robo fainali.

Spain watakuwa wanashuka dimbani majira ya saa 11 jioni kucheza dhidi ya Russia na baadaye majira ya saa 3 usiku, Croatia watakuwa wanacheza dhidi ya Denmark.

Ikumbukwe mshindi wa mechi za leo atakuwa anaungana na Ufaransa pamoja na Uruguay kuelekea robo fainali.

Ufaransa walitinga hatua hiyo kwa kufanikiwa kuwatwanga Argentina jumla ya mabao 4-3 huku Uruguay nayo ikiifunga Ureno kwa mabao 2-1.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic