July 2, 2018


Nyota wa R&B, Ed Sheeran yamemkuta! Unaweza sema hivyo kwa maana nyingine baada ya familia ya aliyekuwa mkali wa muziki huo, marehemu Marvin Gaye kutaka ilipwe dola milioni 100 (zaidi ya bilioni 225 za Kibongo) kwa kosa la kuibiwa wimbo.

Kwa mujibu wa Kampuni ya Structured Asset Sales, inamdai Ed kiasi hicho cha pesa kutokana na kuiba Wimbo wa Let’s Get It On na kuubadili baadhi ya vitu kisha kuuita Thinking Out Loud. Ed anadaiwa kukopi midundo, melodi, sauti pamoja na kiitikio cha mbali kutoka katika wimbo huo uliowahi kuimbwa mwaka 1973.

Mtoto wa Marvin Gaye, Ed Townsend Jr kwa kushirikiana na Structured wameshafikia pazuri ambapo wamewalalamikia makampuni ya Sony/ATV Music, Atlantic Records na mwandishi ambaye ni Ed.Hata hivyo, bado Ed hajatoa ufafanuzi wowote juu ya madai hayo ya kuiba wimbo.

Wimbo wa Thinking Out Loud wa Ed uliachiwa Novemba, 2014 na kuwa namba moja katika chati kubwa duniani za Billboard.

Imeandaliwa na Andrew Carlos/GPL /NEW YORK, Marekani

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic